Placeholder

You are viewing: Hazina Bora

146 KSh
Add to cart

Hazina Bora

Category:

146 KSh

Description

Mwembe ule mzao wake msimu huo ulikuwa mzuri sana. Maembe yalijaa kochokocho katika matawi yake yenye majani ya kijani kibichi. Hakukuwa na haja ya kupambanua baina ya maembe mabichi na mabivu, maana yote pale mwembeni yalikuwa yameiva barabara. Yalikuwa maembe ya kutamanisha sana. Kwa watu waliozaliwa na tamaa kubwa kama mimi, ilikuwa vigumu kujizuia kuyamezea mate.
Mwembe ule aliutunza Mzee Mataka tangu ukiwa mkinda siku za upanzi mpaka kukomaa. Alijishughulisha nao kama mama mzazi ashughulikiavyo mtoto wake mchanga. Aliupalilia na kuunyunyizia maji kwa idili. Na alipoketi kuutazama ulivyonawiri mno na kuzaa maembe chungu nzima, furaha yake haikuwa na kifani. Mzee Mataka mwenyewe alikuwa kafiwa na mkewe karibuni, baada ya miaka mingi ya ndoa ya mapenzi na heri. Alikuwa anautegemea mwembe ule kumruzuku; akiyatunda maembe mawili matatu na kutuuzia sisi wanafunzi shuleni. Hela haba apatazo zikimwezesha kununua angalao kibaba cha unga.

Additional information

Publisher

Author

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Hazina Bora”

Your email address will not be published. Required fields are marked *