Placeholder

You are viewing: Tujivunie Kiswahili Darasa la 6

612 KSh
Add to cart

Tujivunie Kiswahili Darasa la 6

Category:

612 KSh

Description

Kitabu hiki ndicho cha sita katika mfululizo wa vitabu vya Tujivunie Kiswahili. Hiki ni kitabu kinacholenga kuendelea kujenga msingi thabiti wa mwanafunzi wa darasa la sita katika kujifunza Kiswahili, si kwa kuongea tu bali kwa kusoma na kuandika vizuri. Hivyo basi mazoezi kabambe ya kumsaidia mwanafunzi kufikia lengo hili yametolewa kwa njia ya kitaaluma.

Kadhalika mwanafunzi ameelekezwa kwenye maswala ibuka kwa njia ya kuvutia kupitia picha, hadithi, vitendawili na mafumbo, mashairi na michezo ya kuigiza. Isitoshe, kitabu hiki kina mwongozo wa mwalimu ambao umeandikwa kwa njia inayoeleweka kwa urahisi ili mwalimu asitatizike anapoandaa somo.

Kitabu hiki kimeshughulikia mambo mengi, yakiwemo yafuatayo:

silabasi ya darasa la sita
stadi zote za lugha zimeshughulikiwa katika mafunzo yaliyopangwa katika vipindi vitano kila juma
somo la sarufi limezingatia mpangilio rahisi wa kujifunza ngeli
msamiati umezingatia kiwango cha mwanafunzi na hali halisi ya maisha
mazoezi kemkemu yametolewa ili kutathmini maendeleo ya mwanafunzi.

Additional information

Publisher

Author

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Tujivunie Kiswahili Darasa la 6”

Your email address will not be published. Required fields are marked *