Placeholder

You are viewing: Watu wa Gehenna

459 KSh
Add to cart

Watu wa Gehenna

Category:

459 KSh

Description

Watu wa Gehenna ni riwaya ya kimajaribio yenye muundo changamano iliyoandikwa kiginingi na ambayo mtindo unaotumika kuifinyanga unakiuka baadhi ya taratibu na uzoefu wa uandishi wa riwaya. Jambo hili linamtumbukiza msomaji ndani ya tufani inayomzungusha huku na kule kama portangi, bongo lake kutekenywa, uginingi kumfanya kufikia njia panda asijue anatoka ndotoni am a anakwenda Ndotoni – matilabaye ni kuwa msomaji anakosolewa, anachokozwa na anaepuka uwezekano wa kuwa tarakimu katika orodha ya watu wa Gehenna!Ni riwaya ambayo mbali na kusimulia chimbuko la ufisadi, inapiga msasa masuala ibuka, mathalan, biashara haramu ya kuuza nyeti za zeruzeru, kuteswa kwa wafanyakazi wa nyumbani katika mataifa ya ng’ambo na vilevile athari za teknohama katika mitandao ya kijamii hususan Facebook na Twitter. Masimulizi yanafanywa kwa mtindo wa kipekee unaosheheni ugothi, uhalisia wa kiajabu na nguvu za giza.

Additional information

Publisher

Author

Reviews

There are no reviews yet.

Be the first to review “Watu wa Gehenna”

Your email address will not be published. Required fields are marked *